18/11/2025
Leo, tunapoadhimisha Siku ya Kahawa Duniani, tunawaenzi wakulima wetu kwa kuwasaidia kuboresha uzalishaji, kulinda mazingira na kufikia masoko ya Ulaya.
Bizy Tech tunaendelea kuwawezesha wakulima wa kahawa kupitia usajili wa mashamba ya kidijitali na utekelezaji wa matakwa ya EUDR chini ya mradi wa KilimoSoko | Mazingira, hatua muhimu inayofungua milango ya soko la Umoja wa Ulaya.
Kupitia KILIMO BaNDO, wakulima hupata taarifa sahihi, ushauri unaotekelezeka, na mifumo madhubuti ya ufuatiliaji (traceability) kuhakikisha kahawa yao inakidhi viwango vya kimataifa na kupata thamani wanayostahili.