10/12/2015
KUTAMBUA NA KUTATHMINI FURSA ZA BIASHARA.
Nini maana ya Fursa bora?
Mjasiriamali ni mtafutaji fursa. Kazi yake ya kwanza ni kutambua na kuchagua fursa
inayovutia au yenye manufaa. Nini maana ya fursa? Kwa lugha rahisi inaweza ikawa
na maana ya uwezekano wa mradi kufanikiwa.
Utambuzi wa fursa za biashara unahitaji juhudi za ziada na ujuzi maalum. Hta hivyo
kwa wakati wowowte panahitajika vigezo na miongozo itakayosaidia kutambua na
kutathmini fuursa vipo kwenye ngazi ya maeneo husika .Vigezo hivyo ni pamoja na:
A: MAZINGIRA
- Hali halisi ya eneo na rasilimali zilizopo zake.
- Watu, aina za kazi/ajira iliyopo na jamii na hali yao kiuchumi
B: MWONEKANO WA BIASHARA ZILIZOPO.
- Hali halisi ya shughuli za biashara zilizopo katika eneo husika kwa
kuhusiamisha na mwingiliano wa bidhaa kutoka katika maeneo jirani,
uwezo wa soko, mahitaji ya bidhaa na huduma za viwandani.
- Mwelekeo na muundo wa shughuli za kibiashara kwa kuzingatia mahitaji
mapya ya bidhaa na huduma kwa wateja katika eneo husika.
C: WALENGWA (WATEJA).
- Matarajio, uwezo na mapungufu yao.(k.m. vile ujuzi, maarifa/ufahamu, hali
ya kifedha n.k.
YAFUATAYO YANAWEZA KUWA MBADALA WA KUSAIDIA KATIKA KUTABUA FURSA YENYE UWEZEKANO WA KUTEKELEZEKA KATIKA ENEO LOLOTE LILE.
(1) RASILIMALI
Viwanda vinavyojihusisha na madini, kilimo, uvuvi na maliasili nyinginezo..
Bidhaa zinazotokana na masalia/mabaki ya kilimo, miti/mbao na metali.
(2) MUUNGANIKO
Viwanda vinavyotokana na muunganiko mbalimbali k**a vile viwanda
ambavyo malighafi yake yanatokana na masalia ya viwanda vingine au
kiwanda kimoja kutegemea kiwanda kingine kwa malighafi katika
uzalishaji na kinyume chake.
- Miradi inayosaidia maendeleo
- Viwanda vinavyojihusika na uandaaji wa bidhaa zinazosafirishwa
nje au uunganishaji wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi au nje ya
eneo husika.
(3) BITHAA ZIZOSAFIRISWA NJE/BITHAA ZISIZOKAMILIKA ZINAZOINGIZWA KUTOKA NJE.
Kwenye maeneo mengine kuna uwezekano wa baadhi ya bidhaa aidha
kuingia kutoka nje ya nchi au kusafirishwa kwenda nje ya nchi.Bidhaa
za aina hiyo zinatoa fursa nzuri katika kuendeleza tasnia
zinazojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa nje na ndani ya
nchi. kati ya hivi vitu viwili,uingizaji wa bidhaa kutoka nje zisizo kamilika
unatoa fursa nzuri inayovutia katika biashara. Katika hali hii siyo tu
uwepo wa bidhaa ndicho kinachovutia bali pia soko lilishakuwepo.
(4) KUBADILIKA AU KUKUA KWA SOKO.
Baadhi ya wateja(walaji) na bidhaa za viwandani zinaasili ya kukua
kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na uwezo wao wa
kununua, mabadiliko ya mtindo wa maisha au kiwango cha maisha.
(5) BITHAA MUHIMU/MAALUM
- Bidhaa zinatokana na utafiti na ubunifu.
- Bidhaa zitokanazo na ujuzi/maarifa
- Bidhaa zitokanazo na manunuzi ya taasisi/serikali au hosipitali/shule
- Bidhaa zitokanazo na ushirikiano na mataifa/viwanda vya nje
(6) SEKTA YA HUDUMA
- Uanzishwaji wa kitengo cha huduma ya matengenezo na ukarabati
wa nyumba husaidia katika kutoa huduma hiyo viwandani na
majumbani pia